Acts 9:32-37

32 aPetro alipokuwa akisafiri sehemu mbalimbali, alikwenda kuwatembelea watakatifu walioishi huko Lida. 33Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Ainea, ambaye alikuwa amepooza na kwa muda wa miaka minane alikuwa hajaondoka kitandani. 34 bPetro akamwambia, “Ainea, Isa Al-Masihi anakuponya, inuka utandike kitanda chako.” Mara Ainea akainuka. 35 cWatu wote wa Lida na Sharoni walipomwona Ainea akitembea wakamgeukia Bwana.

Petro Amfufua Dorkasi

36 dHuko Yafa palikuwa na mwanafunzi jina lake Tabitha (ambalo kwa Kiyunani ni Dorkasi
Tabitha kwa Kiaramu na Dorkasi kwa Kiaramu yote yamaanisha Paa.
). Huyu alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini.
37 fWakati huo akaugua, akafa na wakiisha kuuosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani.
Copyright information for SwhKC